• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Masumbwi, Kenya: Bondia wa Mexico asema ushindi wa Fatma si halali

  (GMT+08:00) 2018-09-11 09:13:10

  Mwanadada bondia kutoka Mexico, Yamileth Mercado ameeleza sababu ya kushindwa kwenye pambano la jumamosi dhidi ya Fatma Zarika wa Kenya lililofanyika mjini Nairobi kuwa ni uamuzi mbaya wa majaji wa pambano hilo, ambao amedai kuwa hawakutenda haki.

  Katika pambano hilo ambalo, Fatma alitetea mkanda wake wa WBC wa uzito wa Super Bantum wanawake, Fatma alishinda kwa pointi kulingana na majaji, na ulikuwa ushindi wake wa 31 katika mapambano 43 aliyoshiriki.

  Licha ya kutoafiki uamuzi wa majaji, Yemileth aliondoka jana huku akiwashukuru mashabiki wake waliomuunga mkono.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako