• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkakati wa Russia wa "Kutupia macho upande wa mashariki" utakuwa na mustakabali mzuri

    (GMT+08:00) 2018-09-11 17:01:27

    Mkutano wa nne wa Baraza la uchumi la nchi za Mashariki ya Mbali unafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 13 mwezi huu mjini Vladivostok, Russia, na kushirikisha viongozi wa nchi mbalimbali za Asia Mashariki na kaskazini akiwemo rais Xi Jinping wa China, pamoja na ujumbe kutoka zaidi ya nchi 60, ambao umeweka rekodi mpya katika historia ya mkutano huo kwa idadi kubwa ya washiriki na kiwango chake.

    Baraza la uchumi la nchi za Mashariki ya Mbali lilianzishwa kutokana na pendekezo lililotolewa na rais Vladimir Putin wa Russia mwaka 2015. Huu ni moja kati ya maamuzi mbalimbali yaliyotolewa na Russia kuhusu "kutupia macho upande wa Mashariki" ili kukabiliana na kuzorota kwa uhusiano kati yake na Marekani na nchi za Ulaya. Katika miaka ya hivi karibuni, kuna mwelekeo kuwa "Kutupia macho upande wa Mashariki" kumekuwa mkakati wa kitaifa wa Russia katika muda mrefu ujao.

    Hali hii inatokana na kuwa Russia imegundua ushirikiano kati yake na China unaleta faida kubwa. China ikiwa mwenzi mkubwa wa kwanza wa biashara wa Russia, kila mwaka inatuma ujumbe wa ngazi ya juu na wenye idadi kubwa ya watu kushiriki kwenye mkutano wa baraza hilo tangu lilipoanzishwa mwaka 2015, na hatua ya Rais Xi Jinping wa China kushiriki kwenye mkutano wa mwaka huu imeonesha msimamo wa China katika kupenda kushirikiana na nchi za Mashariki ya Mbali.

    Ushirikiano katika maeneo ya Asia Mashariki na Kaskazini una mustakabali mzuri. Makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 35.7 yamesainiwa katika mikutano ya baraza hilo iliyofanyika katika miaka mitatu iliyopita, na thamani hiyo inatazamiwa kuzidi dola za kimarekani bilioni 50 mwaka huu.

    Ukuaji wa uchumi katika maeneo ya Asia na Pasifiki umeleta fursa nyingi za maendeleo. Maeneo ya Asia na Pasifiki yakiwa moja kati ya sehemu zinazopata ongezeko la uchumi kwa kasi zaidi duniani, ni soko kubwa la matumizi ya fedha na chanzo muhimu cha uwekezaji kwa Russia.

    Mkakati wa Russia wa "Kutupia macho upande wa mashariki" hautokani na vikwazo vinavyowekwa na nchi za magharibi, bali kuzorota kwa uhusiano kati yake na nchi za magharibi kumeharakisha hatua yake ya kusonga mbele kwa upande wa mashariki. Hata hivyo, Ulaya bado ni mwenzi muhimu wa biashara wa Russia, mwaka 2017 thamani ya biashara kati ya Russia na nchi za Umoja wa Ulaya ilichukua zaidi ya asilimia 40 ya biashara nje ya Russia. Hivyo "Kutupia macho upande wa mashariki" hakumaanishi kuwa Russia itaacha nchi za magharibi haswa ushirikiano na nchi za ulaya, badala yake Russia itadumisha ushirikiano na pande zote mbili, lakini kutokana na mtizamo wa muda mrefu ujao, upeo wa macho katika upande wa mashariki utakuwa na mustakabali mzuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako