• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanahabari wa China na Afrika wajadili mafanikio ya Baraza la Ushirikiano Kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-11 18:31:39

    Mkutano wa vyombo vya habari vya China na Afrika umehudhuriwa na a waandishi 50 wa habari kutoka nchi 29 za Afrika na zaidi ya waandishi 10 kutoka China.

    Kwenye mkutano huo, Mhariri Mkuu wa Televisheni nchini Mauritania Bw. Enderhemar Ahmedou amesema Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano Kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing umetoa fursa mpya za Maendeleo kwa nchi za Afrika. Mwandishi wa habari wa Gazeti la Le Renouveau la Burundi Bw. Mbonihankuye Vincent amesema Rais Xi Jinping wa China ametaja hatua kubwa nane zinazofuata matarajio ya Waafrika katika nyanja zote za ushirikiano wa China na Afrika.

    Kiongozi wa ofisi inayoshughulikia picha wa Gazeti la L'Union la Gabon Bw. Bandoma Nziengui Jean Brice amesema, jukumu la vyombo vya habari vya China na Afrika ni kuwawezesha watu kuelewa kikamilifu yaliyomo katika Baraza la Ushirikiano Kati ya China na Afrika na ushawishi wake katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako