• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Mabasi ya mikoani Tanzania kuanza safari saa kumi na moja

  (GMT+08:00) 2018-09-11 18:59:52

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, wa Tanzania Atashasta Nditye amesema baada ya wiki mbili mabasi yanayoenda mikoa mbalimbali nchini yataanza safari zake saa kumi na moja alfajiri.

  Nditiye alitoa kauli alipotembelea kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT), Dar es Salaam kisha kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wakiwamo wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa).

  Alisema hakuna sababu ya kuwazuia wamiliki wa mabasi wanaotaka magari yao yaanze safari saa kumi na moja alfajiri ya kwa sababu maeneo mengi ya nchi yapo salama kwa sasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako