• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China akutana na makamu wa rais wa Zanzibar

    (GMT+08:00) 2018-09-12 09:27:47

    Naibu waziri mkuu wa China Han Zheng amekutana na makamu wa rais wa Zanzibar, Tanzania balozi Seif Ali Iddi anayehudhuria Maonyesho ya 15 ya China na Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia ASEAN yanayofanyika kuanzia leo hadi Jumamosi mjini Nanning, kusini mwa China.

    Bw. Han ametoa wito kwa Tanzania kutumia ipasavyo Maonyesho hayo kuhimiza zaidi ushirikiano wa biashara na uwekezaji wa pande mbili na kuingiza uhai mpya katika uhusiano wa pande mbili. Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika iwe na nguvu zaidi baada ya kukamilika kwa mafanikio kwa mkutano wa kilele wa Beijing wa mwaka 2018 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako