• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia zakubaliana kuhimiza ushirikiano wa ngazi ya mikoa

    (GMT+08:00) 2018-09-12 10:31:27

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladmir Putin jana huko Vladivostok walihudhuria mazungumzo ya viongozi wa ngazi ya mikoa kati ya nchi hizo mbili.

    Akizungumza katika mazungumzo hayo, rais Xi Jinping alidhihirisha kuwa China na Russia ni nchi jirani na marafiki muhimu kabisa wa ushirikiano wa kimkakati zenye maslahi mengi ya pamoja. Amesema ni muhimu kuimarisha ushirikiano na kuzidisha mawasiliano pamoja na kukabiliana kwa pamoja na matishio na changamoto kutoka nje na kuhimiza maendeleo na ustawi wa pamoja.

    Akitoa mapendekezo kuhusu ushirikiano wa kimikoa kati ya nchi hizo mbili katika siku za baadaye rais Xi amesema serikali za mikoa zinapaswa kuongeza mpango na uratibu wa pamoja, kuboresha mazingira ya sera, kuhimiza uhusiano zaidi wa kiwenzi na kuweka mazingira mazuri ya kurahisisha uwekezaji kati ya makampuni ya nchi hizo mbili. Aidha zinapaswa kuvumbua mawazo ya ushirikiano, kupanua sekta za ushirikiano, kutafuta na kuhimiza njia mpya ya ushirikiano wa kikanda.

    Rais Xi pia ametoa wito kwa serikali za mikoa kutumia ipasavyo nguvu zao na sifa zao maalumu, kusukuma mbele njia za ushirikiano kwa usahihi zaidi, na pia kuimarisha mawasiliano kati ya watu na watu na utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako