• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Netiboli, Ligi Kuu Tanzania: Uhamiaji yashinda ubingwa wa msimu huu

  (GMT+08:00) 2018-09-12 11:18:08

  Timu ya Mamlaka ya Uhamiaji ya Tanzania, imeshinda ubingwa wa ligi ya netiboli kwa kufikisha alama 18 ikiwa imeweka rekodi ya kutopoteza hata mchezo mmoja katika tisa ilizocheza.

  Ligi hiyo ilianza Septemba 4 mjini Mwanza, na ilishirikisha timu 10, na nafasi ya pili ilichukuliwa na timu ya JKT Mbweni ambao ndiyo walikuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo waliojikusanyia alama 16 pekee.

  Nafasi ya tatu ilikwenda kwa timu ya Magereza iliyokusanya alama 14, nafasi ya nne walikuwa ni Polisi Morogo kwa alama 12.

  Mchezaji bora wa ligi hiyo alitangazwa Asha Said kutoka timu ya Jiji la Tanga licha ya kuwa timu yake ilikamata nafasi ya sita na mfungaji bora akiwa ni Fatuma Matenga kutoka Uhamiaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako