• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Kituo kikuu cha radio na televisheni cha taifa ahutubia Baraza kuhusu "Mustakabali wa vyombo vya habari barani Asia vinavyokabiliwa na mageuzi ya kisiasa na kiuchumi"

    (GMT+08:00) 2018-09-12 16:57:05

    Mkuu wa Kituo kikuu cha radio na televisheni cha taifa Bw. Shen Haixiong akishiriki kwenye baraza kuhusu "Mustakabali wa vyombo vya habari barani Asia vinavyokabiliwa na mageuzi ya kisiasa na kiuchumi" lililo chini ya mfumo wa Mkutano wa 4 wa Baraza la uchumi la Mashariki, ametoa pendekezo kwamba, vyombo vya habari vya nchi za Asia vinatakiwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika zama mpya, ili kutoa sauti ya Asia kwa pamoja.

    Bw. Shen ameeleza kuwa, huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mchakato wa mageuzi nchini China katika miaka 40 iliyopita yanategemea sana ushirikiano kati ya nchi mbalimbali barani Asia na dunia nzima. Nadharia na fikra muhimu mbalimbali zinazohusiana mustakabali wa binadamu zilizotolewa na rais Xi Jinping wa China zikiwa ni pamoja na "Kujenga jumuiya ya Asia na binadamu yenye hatma ya pamoja", na pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja", zimeonesha busara ya China. Pia Bw. Shen amesisitiza kuwa vyombo vya habari vinabeba majukumu muhimu katika kuwahimiza watu wa nchi mbalimbali barani Asia kushiriki katika jumuiya yenye hatma ya pamoja, na kuonesha busara na nguvu kwa ushirikiano wa pamoja.

    Bw. Shen pia ameeleza kuwa, nadharia ya kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja, na utoaji na utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" zimehimiza upeo wa macho na nadharia kuhusu ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya nchi za Asia hadi katika kiwango kipya. Kadiri nchi mbalimbali za Asia zinavyojiendeleza, ndivyo hadhi zao katika muundo wa siasa na uchumi duniani zinavyoimarishwa kwa udhahiri. Lakini wakati huo huo, Asia bado ina hadhi ya chini kwenye muundo huo. Hali ambayo imetoa madai mengi kwa ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya nchi za Asia. Pia ametoa mapendekezo kuhusu ushirikiano kati ya vyombo vya habari ili kukabiliana na mageuzi ya muundo wa dunia: Kwanza, kuweka kanuni za ushirikiano, ili kuinua kiwango cha ushirikiano wa kimkakati kati ya vyombo vya habari. Pili kutoa kipaumbele kufanya uvumbuzi, na kukuza ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya aina mpya. Tatu kusukuma mbele uenezi wa habari kwa kufanya ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako