• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya 15 ya China-ASEAN yafunguliwa huko Nanning

    (GMT+08:00) 2018-09-12 17:11:28

    Maonesho ya 15 ya China na Umoja wa nchi za Asia Kusini Mashariki ambayo pia ni mkutano wa kilele wa biashara na uwekezaji kati ya China na nchi za ASEAN yamefunguliwa leo huko Nanning, Guangxi nchini China.

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, maonesho hayo ya siku nne yameshirikisha kampuni 2,700 kutoka nchi 29 za Ukanda Mmoja na Njia Moja zikiwemo nchi 10 za Umoja wa Asia Kusini Mashariki. Licha ya China na nchi za Umoja wa Asia Kusini Mashariki, maonesho hayo pia yamevutia kampuni 114 kutoka nchi 19 za Ukanda Mmoja wa Njia Moja zikiwemo Tanzania, Sri Lanka, Pakistan, Nepal, Australia, Ujerumani, Italia na Hispania.

    Bw. Gao Feng amesema, tangu maonesho hayo yalipoanzishwa miaka 14 iliyopita, yamehimiza ushirikiano kati ya China na Umoja wa nchi za Asia Kusini Mashariki kwenye sekta kadhaa ikiwemo biashara na uwekezaji, fedha, forodha, na sayansi na teknolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako