• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Kenya wateta kuhusu sukari ghushi

    (GMT+08:00) 2018-09-12 18:49:39

    Mjadala mkali umeibuka nchini Kenya baada ya madai kwamba shughuli za kampuni ya sukari Mumias Sugar na zinginezo zinatatizwa na wakiritimba wanaothubutu kupakia sukari ya magendo kwa pakiti zenye nembo ya Mumias Sugar. Wabunge wa Kenya wametaja sukari hiyo kuwa "ghushi na hatari", wakiteta imesambaa nchini Kenya na ndiyo 'inaua' kiwanda hicho.

    Kwenye kikao na waandishi wa habari, wabunge hao walitaka kujua jinsi ambavyo sukari hiyo iliingia nchini na kupakiwa kwa nembo ya kiwanda hicho.

    Miezi kadha iliyopita serikali ilifanya msako dhidi ya sukari hatari, iliyosemekana kuwa na madini ya Lead na Copper, iliyopatikana ikipendekezwa kuchomwa.

    Wabunge hao wanasisitiza kuwa sukari hiyo ingali sokoni, na ndiyo inapakiwa kwa nembo ya Mumias Sugar.Wabunge hao wamesema sukari bandia ikiondolewa nchini K enya, kampuni za kusaga sukari zitaimarika ambapo wakulima wa miwa wataweza kuwa na ari ya kuendelea kukuza miwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako