• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viwanda vya sukari hatarini kufungwa Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-09-12 18:50:15

  Endapo Serikali ya Tanzania haitadhibiti biashara ya magendo ya sukari, viwanda vya Kagera na Mtibwa vimesema vitalazimika kusitisha uzalishaji.

  Hatua hiyo inatokana na viwanda hivyo kuwa na shehena kubwa ya sukari iliyozalishwa ambayo inakosa soko, jambo linalohatarisha operesheni zao na kutishia ajira za maelfu ya wafanyakazi iwapo vitafungwa.

  Meneja uendeshaji wa viwanda vya Kagera na Mtibwa Abel Magese amesema soko limekuwa gumu kutokana na sukari kutoka nje ya nchi kuingizwa kwa njia za panya.

  Novemba 2017, Rais John Magufuli alibatilisha utaratibu wa utoaji wa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje akitaka kulinda viwanda vya ndani.

  Rais alimwagiza Waziri wa Kilimo kuivunja menejimenti ya Bodi ya Sukari na kuwapangia watendaji wake kazi nyingine.

  Alichukua uamuzi huo ukiwa ni mwaka mmoja tangu alipozuia uagizaji wa sukari isipokuwa kwa kibali maalumu. Kwenye mabadiliko hayo, Rais aliagiza wazalishaji wapewe vibali vya kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje.

  Baada ya njia hizo halali kubanwa, baadhi ya wafanyabiashara wanaendelea kuagiza bidhaa hiyo bila kufuata utaratibu uliopo, hivyo kuviumiza viwanda vya ndani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako