• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kutathmini sheria ya kudhibiti vyama vya ushirika

  (GMT+08:00) 2018-09-12 18:50:43

  Waziri wa Viwanda na Biashara wa Kenya Bw Peter Munya amesema kuwa serikali inatathmini upya sheria ya kudhibiti vyama vya ushirika.

  Amesema kuwa sheria hiyo itatilia mkazo kuchipuka kiholela kwa mashirika hayo mashinani yakijificha chini ya leseni za serikali za kaunti. Amesema kuwa sheria hizo zinalenga kupokonya serikali za Kaunti uwezo wa kusajili mashirika hayo bila idhini ya serikali kuu.

  Amesema hatua hiyo itakuwa inalenga kuwalinda wanaohifadhi pesa zao katika mashirika hayo ya akiba na mikopo.

  Katika sheria hizo, kutaundwa halmashauri ya Umoja wa Mashirika hayo na ambayo yatashinikizwa kuweka kitita cha Sh10 milioni kila mmoja na ambacho kitatumika kugharamia hasara ya waweka hazina ikiwa shirika hilo litasambaratika. Munya amesema mpangilio huo ni wa kuzima njama kama zilizoundwa na matapeli chini ya mpangilio wa Deci na ambapo Wakenya takriban 2,000 walipoteza akiba zao zinazokadriwa kuwa Sh30 bilioni.

  Amesema kuwa mswada wa kuunda halmashauri hiyo tayari umeanza kufanyiwa kazi na utakamilika kabla ya mwaka huu na kutekelezwa baada ya kupitishwa bungeni. Alisema kuwa halmashauri hiyo itakuwa na wajibu wa kuunganisha mashirika yote katika Kaunti na kuyaweka chini ya utaratibu na uthibiti wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako