• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping arudi Beijing baada ya kuhudhuria kongamano la 4 la uchumi wa Mashariki nchini Russia

    (GMT+08:00) 2018-09-13 09:50:11

    Rais Xi Jinping wa China jana usiku alirudi Beijing baada ya kuhudhuria kongamano la 4 la uchumi wa mashariki nchini Russia.

    Kabla ya hapo, rais Xi Jinping na mwenzake wa Russia Vladmir Putin walitembelea kituo cha watoto cha Ocean cha Russia na kuhudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya kupokea watoto wa China waliokumbwa na tetemeko la ardhi la Wenchuan.

    Rais Xi Jinping amesema, wanafunzi 996 wa China waliokumbwa na tetemeko la ardhi la Wenchuan walialikwa kwenda kituo hicho kupata mapumziko. Amesema, historia ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia pia ni historia ya mawasiliano kati ya vijana wa nchi hizo mbili. Katika miaka ya hivi karibuni, mawasiliano kati ya vijana wa China na Russia yamekuwa ya karibu zaidi, na kuongeza maelewano na urafiki kati yao.

    Rais Xi pia anatumai vijana wa nchi hizo mbili wataimarisha maingiliano, kufunzana, na kushirikiana kurithi urafiki kati ya China na Russia.

    Naye rais Putin amesema, maingiliano ya kirafiki kati ya vijana wa nchi hizo mbili yameweka msingi imara zaidi wa uhusiano wa pande mbili, na kwamba ni muhimu kwa mustakabali wa uhusiano kati ya Russia na China. Pia anatumai kuwa vijana wa Russia na China wataenzi urafiki wa watu wa nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako