• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Misri asema ushirikiano kati ya China na Afrika umeleta ushawishi na hamasa kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-09-13 18:16:51

    Balozi wa China nchini Misri Bw. Song Aiguo, amesema China na Afrika zinapinga kithabiti utaratibu wa upande mmoja, na vitendo vya kujilinda kibiashara, huku ikilinda kithabiti utaratibu wa pande nyingi na biashara huria, hali ambayo imeleta ushawishi na hamasa kwa jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Song aliaambatana na rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri na kuhudhuria mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu hapa Beijing. Amesema viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika walioshiriki kwenye mkutano huo wamesifu urafiki wa jadi kati ya China na Afrika baada ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali duniani, pamoja na juhudi za rais Xi Jinping wa China katika kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili na majukumu muhimu China inayobeba. Pia wameishukuru China kwa kuisaidia Afrika kuondokana na umaskini na kutimiza maendeleo endelevu, na kusema China ni mwenzi wa kuaminika katika kulisaidia bara la Afrika kujiendeleza na kupata ustawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako