• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu asema mkutano wa kilele wa FOCAC umefungua safari mpya kwa ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-13 19:45:23

    Mkuu wa Taasisi ya utafiti kuhusu mambo ya Afrika kwenye Chuo cha utafiti kuhusu uhusiano wa kisasa wa kimataifa cha China Bw. Xu Weizhong amesema, mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu hapa Beijing unafuata hali na umaalumu mpya wa maendeleo ya nchi za Afrika, na kufungua safari mpya katika kufanya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Xu amesema, mkutano huo umetoa kipaumbele kwa wazo la kunufaishana, na kuthibitisha lengo la kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika, pia kuweka mipango ya utekelezaji katika sekta nane muhimu za ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika miaka mitatu ijayo. Hatua hiyo ina umuhimu mkubwa katika kukuza ushirikiano kati ya China na Afrika na kuimarisha ushirikiano kati ya Kusini na Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako