• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EAC:Umoja wa Ulaya wamepndekeza muungano mpya wa Afrika

  (GMT+08:00) 2018-09-13 20:10:51

  Rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker amependekeza kuwepo kwa muungano mpya na Afrika, kuboresha uhusiano wa kiuchumi na pia kuongeza uwekezaji na ajira.

  Kwenye hotuba yake ya kila mwaka Bw Juncker alisema mpango huo utasaidia kubuniwa mamilioni ya ajira barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano inayokuja.

  Maoni ya Bw Juncker yanahusu kile anachokiita biashara huru kati ya mabara.

  Ametaja Suala la kuboresha mikatati iliyopo sasa ambayo inazipa karibu nchi zore za Afrika uwezo wa kufikia masoko ya Ulaya bila kodi.

  EU inapendekeza Jumla ya euro bilioni 40 katika kipindi cha miaka saba hadi mwaka 2021.

  Pia Juncker alitangaza mipango ya EU kutuma walinzi wa mipaka 10,000 kukabiliana na uhamiaji haramu ifikapo mwaka 2020. Bw Jucker alisema EU inahitaji kuwa salama kutoka kwa vitisho vingi vinavyoikumbwa.

  Mashirika ya Frontex na lile na ulinzi wa mipaka na pwani la Ulaya kwa sasa yamewajiri walinzi 1,600 kutoka Ulaya, kwa hivyo idadi mpya inayotajwa na Juncker ni ongezeko kubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako