• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa Ethiopia ahimiza utulivu baada ya vurugu kutokea Addis Ababa

  (GMT+08:00) 2018-09-14 09:58:58

  Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amehimiza kurudisha utulivu baada ya kutokea kwa vurugu mjini Addis Ababa kutokana na bendera yenye utata, na vurugu hizo zimesababisha majeruhi ya watu kadhaa.

  Vurugu hizo zilianza Jumatano baada ya wafuasi wa kundi la zamani la waasi la OLF ambao wengi wao wanatoka vijiji vya kabila la Oromo, kuingia mjini Addis Ababa wakipeperusha bendera ya OLF, na kupambana na wakazi wa mji huo.

  Bw. Ahmed amesema Waethiopia wana uhuru wa kutoa maoni yao, ikiwemo kubeba bendera wanayoipenda, lakini amesisitiza kuwa hakutakuwa na mshindi yeyote katika mapambano yanayosababishwa na bendera, na watu wanapaswa kushirikiana na kutatua maoni tofauti kupitia mazungumzo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako