• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maafisa wa FERWAFA wakamatwa kwa tuhuma za madai ya rushwa waliyofunguliwa na refa Pavaza kabla ya mechi ya Rwanda na Ivory Coast

  (GMT+08:00) 2018-09-14 10:40:01

  Maafisa wawili wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Rwanda (FERWAFA) wamenashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi kwa kosa la kutaka kumpa rushwa mwamuzi toka nchini Namibia Jackson Pavaza.

  Paraza aliwashitaki viongozi hao kutaka kumhonga kabla ya mechi ya Rwanda na Ivory Coast wiki iliyopita.

  Pavaza ameeleza hayo kupitia vyombo vya habari vya nchini Namibia na kusema kuwa kabla ya mechi iliyomalizika Rwanda ikikubali kichapo cha 2-1 kutoka Ivory Coast, uwanja wa Kigali Jumapili ya wiki iliyopita, katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Rwanda na Ruhumuriza Regis ambaye anashugulika na mashindano katika shirikisho hilo walitaka kumpa rushwa lakini alikataa.

  Shirikisho hilo awali lilikanusha vikali tuhuma hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako