• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanariadha wanane kuiwakilisha Tanzania, mashindano ya Jumuiya ya Madola

  (GMT+08:00) 2018-09-14 10:40:31

  Tanzania itawakilishwa na wanariadha wanane katika mashindano ya riadha ya nusu marathoni yanayotazamiwa kufanyika Oktoba 7 katika Mji wa Cardiff nchini Uingereza.

  Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Shirikisho la mchezo wa riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabudai mashindano hayo ya nusu marathoni ni ya kwanza kuandaliwa na Jumuiya ya Madola.

  Hata hivyo Tanzania, itakabiliwa na kibarua pevu kuwania medali katika mashindano hayo, kutokana na uwepo wa wanariadha kutoka mataifa ya Kenya na Afrika Kusini ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako