• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano kati ya China na Russia waendelea vizuri chini ya uongozi wa kirais na juu ya msingi wa kiraia

    (GMT+08:00) 2018-09-14 14:45:36

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Bw. Vladmir Putin walikutana tena hivi karibuni katika kongamano la nne la uchumi wa sehemu za Mashariki. Katika miaka mitano iliyopita, marais hao wawili walikutana kwa mara zaidi ya 20. Hali hii imeonesha umuhimu wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Chini ya uongozi wa marais hao wawili, uhusiano wa wenzi na ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Russia umeingia katika zama mpya, na ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, nishati, mawasiliano ya barabara, ujenzi wa miundo mbinu, anga ya juu, sayansi na teknolojia, kilimo, biashara ya mtandao wa Internet na nyinginezo umesukumwa mbele hatua kwa hatua.

    Wakati huo huo, mawasiliano ya watu wa China na Russia pia yameendelea vizuri. Mwezi Julai mwaka jana, marais wa nchi hizo mbili waliposaini Taarifa ya Pamoja ya Kukuza zaidi Uhusiano wa Wenzi na Ushirikiano wa Kimkakati kati ya China na Russia walisisitiza kuwa, maelewano ya watu na mawasiliano ya utamaduni ni msingi wa urafiki wa kizazi baada ya kizazi kati ya nchi hizo mbili.

    Mwaka jana, idadi ya Wachina waliotalii nchini Russia ilifikia milioni 1.7, huku idadi ya Warussia waliotalii nchini China ikizidi milioni 2.3. Hadi mwaka 2016, idadi ya jumla ya wanafunzi wa China wanaosoma nchini Russia na wanafunzi wa Russia wanaosoma nchini China ilizidi elfu 70.

    Uhusiano kati ya China na Russia ni mfano mzuri kwa nchi kubwa na nchi jirani. Kama waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alivyosema, chini ya uongozi wa marais, mawasiliano mazuri ya watu yatakuwa chanzo cha maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako