• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yarekebisha Makubaliano ya Karne

  (GMT+08:00) 2018-09-14 16:51:59

  Mwakilishi maalumu wa rais wa Marekani kwenye mazungumzo ya kimataifa Bw. Jason Greenblatt amesema, Makubaliano ya Karne yanayopangwa kwa ajili ya kuzihimiza Palestina na Israel zitimize amani, yanarekebishwa kwa mara ya mwisho kabla ya kutangazwa.

  Gazeti la New York Times la nchini humo limemnukuu Bw. Greenblatt akisema, Marekani inaona kuwa makubaliano hayo yanaweza kuzinufaisha pande mbalimbali, na nchi hiyo iko tayari kupokea malalamiko kutoka pande mbalimbali. Lakini amekataa kueleza kwa undani makubaliano hayo yatatangazwa lini na mambo muhimu ya makubaliano hayo.

  Tangu rais Donald Trump aingie madarakani, alianza kutekeleza utungaji wa makubaliano hayo, lakini Palestina imesema haitayakubali kwani hayajadili masuala muhimu ya Jerusalem, wakimbizi Wapalestina na ujenzi wa makazi ya Wayahudi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako