• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisa wa G77 apongeza China kwa kupaza sauti ya nchi zinazoendelea

  (GMT+08:00) 2018-09-14 16:56:41

  Mwenyekiti wa Kundi la nchi 77 tawi la Vienna Bw Carlos Jativa, ameipongeza China kwa kuliunga mkono kundi hilo na kupaza sauti ya nchi zinazoendelea katika kushughulikia mambo ya kimataifa.

  Katika maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa kundi hilo, Bw Jativa amesema, hali ya kisiasa duniani imekumbwa na mabadiliko makubwa toka kuanzishwa ofisi za kundi hilo Geneva, na hivi sasa China inafanya kazi muhimu katika mambo ya kimataifa. Amesema China, ambayo ni nchi shiriki muhimu ya kundi hilo, inaziunga mkono nchi zinazoendelea, hali inayochangia kupaza sauti ya nchi hizo. Pia amesisitiza kuwa, pande hizo mbili zitaendelea kulinda na kuenzi siasa ya kushirikisha pande zote.

  Kundi la nchi 77 lililoanzishwa mwaka 1964, ni jumuiya muhimu inayosawazisha misimamo ya nchi zinazoendelea katika mambo ya kimataifa na katika mashirika mbalimbali ya kimatiafa ukiwemo Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako