• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaahidi kuchangia kazi ya uondokanaji umaskini duniani

  (GMT+08:00) 2018-09-14 16:57:09

  China imeahidi kuongeza juhudi na kutoa msaada kwa ajili ya kazi ya kuondokana na umaskini duniani.

  Hayo yamesemwa na balozi wa China kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Yu Jianhua katika kikao cha kujadili kuondokana na umaskini na haki za binadamu kilichoandaliwa kwa pamoja na China na Afrika Kusini huko Geneva, Uswisi. Balozi Yu amesema, China inatoa kipaumbele kwa haki za kuishi na kujipatia maendeleo, na imepata mbinu na uzoefu katika kupambana na umaskini. Pia China imetunga mpango kabambe utakaowaondoa wanavijiji wanaothibitishwa kuwa maskini kutokana na viwango vilivyopo ifikapo mwaka 2020. Ameongeza kuwa, nyaraka mbili zilizopitishwa kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika wiki iliyopita hapa Beijing, zimebainisha njia halisi ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuchangia kazi ya kuondokana na umaskini na maendeleao barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako