• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Korea Kaskazini yatoa wito kutekeleza kikamilifu Azimio la Panmunjom

  (GMT+08:00) 2018-09-14 17:20:26

  Gazeti la Kamati kuu ya Chama cha wafanyakazi cha Korea Kaskazini Rodong Simun limetoa makala ikisisitiza kuwa, kutekeleza kikamilifu Azimio la Panmunjom ni njia muhimu katika kuboresha na kukuza uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

  Makala hiyo imesema, kusainiwa kwa Azimio la Panmunjom na mazungumzo na mawasiliano yanayofanyika kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini yameleta uwezekano na kuweka msingi kwa ajili ya kuhimiza maendeleo mapya kati ya pande hizo mbili. Utekelezaji mzuri wa azimio hilo ni njia muhimu katika kupunguza hali ya kutoaminiana na mvutano kati ya pande hizo mbili. Kutokana na hali ya sasa, pande hizo mbili zinatakiwa kujiamulia mustakabali wao na kutatua masuala yaliyopo kwenye uhusiano kati yao kwa kujitegemea.

  Viongozi wa nchi hizo mbili Kim Jong Un na Moon Jae In walisaini azimio hilo mwezi Aprili mwaka huu, na wanatarajia kukutana kwa mara ya tatu huko Pyongyang, Jumanne hadi Alhamisi wiki ijayo. Viongozi hao watajadili utekelezaji wa azimio hilo, hususan mpango halisi wa kuifanya Peninsula ya Korea iwe eneo lisilo na silaha za nyuklia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako