• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping apongezwa kwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Uchumi la Mashariki

  (GMT+08:00) 2018-09-14 18:25:40

  Katibu mkuu wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Bw. Anton Kobyakov amesema, rais Xi Jinping wa China kushiriki kwenye baraza hilo kumeweka nguzo mpya katika maendeleo ya uhusiano kati ya Russia na China. Naye naibu mkuu wa Taasisi ya masuala ya Mashariki ya Mbali kwenye Chuo cha Sayansi cha Russia Bw. Adrei Ostrovsky amesema, mazungumzo kati ya viongozi wa Russia na China yatazidi kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, hususan uhusiano wa kiuchumi na kibiashara. Mwanauchumi wa Japan Bw. Hidetoshi Tashiro amesema, kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya nchi mbalimbali za Asia Kaskazini Mashariki unasaidia ustawi na utulivu kwenye kanda hiyo. Ana matumaini kuwa mkutano huo utapiga hatua muhimu katika kufungua ukurasa mpya kwa ushirikiano kati ya Japan na China.

  Akiwa nchini Russia, rais Xi na rais Vladimir Putin wa Russia waliweka mipango kuhusu ushirikiano wenye ufanisi kati ya pande hizo mbili katika kipindi kijacho, na kujadiliana na nchi mbalimbali za Asia Kaskazini Mashariki kuhusu mipango ya amani na maendeleo ya kikanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako