• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tume ya Ulaya yalenga kubuni ajira milioni 10 barani Afrika

  (GMT+08:00) 2018-09-14 19:12:10

  Rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker amependekeza kuwepo kwa muungano mpya na Afrika, kuboresha uhusiano wa kiuchumi na pia kuongeza uwekezaji na ajira.

  Kwenye hotuba yake ya kila mwaka Bw Juncker amesema mpango huo utasaidia kubuniwa mamilioni ya ajira barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano inayokuja.Maoni ya Bw Juncker yanahusu kile anachokiita biashara huru kati ya mabara. "Suala hapa ni kuboresha mikatati iliyopo sasa ambayo inazipa karibu nchi zore za Afrika uwezo wa kufikia masoko ya Ulaya bila kodi."

  Pendekezo hilo pia linawapa fursa zaidi watu kutoka afrika kuongeza maarifa kwa mfano kwa kusomea viuo vikuu vya Ulaya.EU inapendekeza Jumla ya euro bilioni 40 katika kipindi cha miaka saba hadi mwaka 2021.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako