• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bodi ya Nafaka ya kitaifa kwenda hasara kutokana na uharibu wa mahindi

  (GMT+08:00) 2018-09-14 19:13:21

  Bodi ya Nafaka ya kitaifa nchini Kenya huenda ikaenda hasara ya shilingi bilioni 8.5 kutokana na kuharibika wa mahindi mwaka mmoja tu baada ya kununuliwa kutoka kwa wakulima. Kaimu mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw Alvin Sang amesema bodi ya kuweka mikakati ya hifadhi ya chakula SFR imeshindwa kutekeleza jukumu lake jambo ambalo limepelekea kushindwa kufikiwa kwa uamuzi wa kuuza jumla ya magunia milioni 3.6 za mahindi na kufanya mahindi hayo kuwa katika hatari ya kuharibika. Bw Sang amesema wangependa kupewa idhini na SFR kupakia upya mahindi ambayo hayajaharibika ili kuzuia mahindi yote kuharibika. Hii ni baada ya baadhi ya mahindi kuonekana kubadilika rangi hadi ile njano na ya kahawa.Sang amesema kuna soko kubwa sana la mahindi mjini Kisumu na iwapo watapewa idhini na SFR watasafirisha mahindi kwa wenyeji wa Kisumu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako