• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tamasha la tatu la Vijana wa Asia na Afrika lafanyika mjini Beijing

  (GMT+08:00) 2018-09-14 20:05:52

  Tamasha la tatu la Vijana wa Asia na Afrika lililoandaliwa na Kamati Kuu ya Vijana ya chama cha Kikomunisti na Shirikisho la Vijana la Taifa limefanyika hapa mjini Beijing, na mada kuu iliyojadiliwa ni umoja, urafiki na ushirikiano.

  Tamasha hilo limehudhuriwa na wawakilishi mia 300 kutoka nchi 50 za Asia na Afrika, wanafunzi wa Asia na Afrika wanaosoma hapa China, pamoja na vijana kutoka China. Washiriki hao wamefanya shughuli mbalimbali ikiwemo baraza la mawasiliano, mihadhara, maonyesho ya utamaduni, na kubadilishana uzoefu. Lengo la tamasha hilo ni kuwa mrithi wa urafiki wa jadi wa Asia na Afrika na kufungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa Asia na Afrika.

  Kwenye hafla ya ufunguzi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Vijana ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Li Keyong amesema, katika miaka 60 iliyopita, viongozi wa vizazi vya zamani wa nchi za Asia na Afrika walikusanyika katika mkutano wa Bandung na kuthibitisha lengo ya mkutano huo, ambalo ni "umoja, urafiki na ushirikiano," ili kuhimiza zaidi mchakato wa uhuru wa bara la Asia na Afrika, na watu wa Asia na Afrika hatua kwa hatua walipata hatma yao wenyewe. Leo, ili kukabiliana na fursa na changamoto mpya, nchi za Asia na Afrika zinaendelea kushikilia azimio la Bandung, kusaidiana, kushikamana, kushirikiana na kunufaishana ili kuandika ukurasa mpya wa ushirikiano wa Asia na Afrika. Amewataka vijana wa Asia na Afrika kujenga makubaliano, kuwa warithi wa urafiki wa Asia na Afrika, kuwa wenzi wa ushirikiano, na wanaohimiza maendeleo endelevu. Pia amewahimiza vijana hao kuchukua nafasi yao katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kujiunga na mambo ya ushirikiano wa Asia na Afrika na kujenga pamoja jamii bora.

  Katibu Muu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) cha Tanzania anayeshughulikia na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Bw. Mohamed Aliani Abdallah ameeleza matumaini yake kuwa, Tamasha la Vijana la Asia na Afrika la mwaka 2018 litakuza ushirikiano kati ya vijana wa China, Afrika na nchi nyingine za Asia, hasa katika mafunzo ya uongozi, elimu ya juu, maendeleo na uwekezaji, na utalii.

  Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Vijana la Asia Bw. Many Hun amepongeza wazo la Rais Xi Jinping wa China la kufanya tamasha hilo, na anatumaini vijana walioshiriki wataelewa utamaduni wa kila mmoja na mustakabali wa siku za mbele, ili kukuza urafiki kati ya mabara mawili ya Asia na Afrika, kuunda dunia ya amani, imara na yenye ustawi zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako