• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washauri mabingwa watoa wito wa kuimarishwa ushirikiano katika sekta ya elimu kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-15 18:48:03
    Jopo la washauri mabingwa kutoka China limetoa wito wa kufanyika juhudi zaidi za kuinua kiwango cha mabadilishano na ushirikiano wa kielimu kati ya China na Afrika.

    Wito huo umechapishwa katika ripoti iliyotolewa wiki hii na Taasisi ya elimu ya maendeleo ya jamii ya China, ambayo pia ilipendekeza kuwa ni vyema baraza la mawaziri wa elimu kutoka China na Afrika lifanyike mara kwa mara na liimarishwe.

    Ripoti hiyo pia imesisitiza kuwa ni muhimu kuimarisha wajibu wa serikali na kutoa mapendekezo ya kuzifanya baadhi ya shule na asasi za kielimu kushiriki kuvutia sekta na jumuiya za kijamii.

    Mbali na kusaidia elimu barani Afrika, pia ilipendekeza elimu iwe katika mfumo unaoendana na mahitaji ya soko pamoja na soko la uwekezaji barani Afrika ili kufikia lengo la kunufaika kwa pamoja.

    Kwa kutambua mafanikio yaliyopatikana kwenye ushirikiano wa kielimu kupitia wanafunzi wa kigeni, ushirikiano baina ya vyuo na vyuo vya mafunzo ya ufundi, pia ikitaja idadi ndogo ya wanafunzi kutoka China wanaosoma Afrika.

    Hivyo pamode zote zinapaswa kuweka mazingira wezeshi na fursa kwa watu kutoka pande zote kubadilishana ziara na masomo katika kila upande ili kuongeza wataalam zaidi China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako