• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalalamikia raia wake kutendwa vibaya na polisi nchini Sweden

    (GMT+08:00) 2018-09-15 20:42:38

    China imetoa taarifa ikieleza kushangazwa na kukasirishwa na polisi wa nchini Sweden kuwatenda vibaya raia watatu wa China, na imelaani vikali kitendo hicho.

    Mkurugenzi wa ofisi ya ubalozi wa China nchini Sweden Bw. Zhang Lei amesema, ubalozi huo na wizara ya mambo ya nje ya China zimetoa malalamiko kwa serikali ya Sweden, na kusisitiza kuwa kitendo hicho cha polisi wa Sweden kimedhuru usalama wa maisha na haki za binadamu za raia hao wa China, na kuitaka serikali ya Sweden kulichunguza tukio hilo mara moja.

    Habari zinasema wachina hao watatu ambao ni familia moja alfajiri ya tarehe 2 mwezi huu walifika nchini Sweden kufanya utalii, na walibishana na wafanyakazi wa hoteli yao baada ya kukataliwa kupewa vyumba. Polisi waliwashikilia kimabavu garini na kuwashusha kwenye makaburi yaliyoko mbali na mji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako