• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 10 wa uwekezaji wa China katika nchi za nje wafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-09-16 18:34:42

    Mkutano wa 10 wa uwekezaji wa China katika nchi za nje umefunguliwa jana hapa Beijing, na utajadili masuala ya ushirikiano wa kimataifa wa nishati na usuluhishi wa mikwaruzano ya uwekezaji kutokana na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Kauli mbiu ya mkutano huo ni kuvumbua njia ya uwekezaji katika nchi za nje, na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia". Kwenye mkutano huo, ofisa wa kamati kuu ya mageuzi na maendeleo ya China Bw. Wang Jianjun ameeleza hali ya uchumi nchini China, na kujumuisha mafanikio yaliyopatikana tangu China itoe pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Amesema China inahamasisha kampuni zake kufanya uwekezaji katika nchi za nje, na pia inatumai nchi zinazohusika zitatoa mazingira mazuri zaidi kwa kampuni hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako