• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpira wa Wavu: Rwanda yatinga nusu fainali klabu bingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-17 10:12:56

    Kwa kuifunga timu ya taifa ya Cameroon, timu ya taifa ya Rwanda ya mchezo wa mpira wa wavu imefanikiwa kutinga nusu fainali ya ubingwa wa Afrika kwa timu za vijana chini ya umri wa miaka 21.

    Aidha Rwanda ilifanikiwa kushinda mechi mbili dhidi ya Nigeria na Cameroon na ikiwa imepoteza moja dhidi ya Tunisia.

    Katika hatua ya nusu fainali, Rwanda itavaana na Misri wakati Tunisia watacheza dhidi ya Morrocco.

    Timu mbili za juu ndizo zitakazoliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya Kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 hapo mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako