• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Magari: Hamilton ashinda michuano ya Singapore

    (GMT+08:00) 2018-09-17 10:13:49

    Dereva Lewis Hamilton wa Uingereza amefanikiwa kujiongezea nafasi ya kushinda ubingwa wa mashindano ya magari ya mwendokasi kwa msimu huu kutokana na ushindi aliopata jana kwenye mbio za Singapore.

    Kwenye msimamo mpaka sasa, Hamilton amefikisha alama 181 ambazo ni 40 zaidi ya mtu wa pili, na huu ni ushindi wake wa saba katika mbio 14 zilizofanyika msimu huu.

    Mshindi wa pili katika mbio hizo za jana alikuwa ni Mholanzi Max Verstappen wa timu ya Redbull na nafasi ya tatu ikienda kwa mpinzani wa karibu wa Hamilton, Sebastian Vettel wa timu ya Ferrari.

    Madereva hao sasa wanajiandaa na mbio za Urusi zitakazofanyika Septemba 30 mjini Sochi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako