• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riadha, Marathon: Kipchoge wa Kenya aandika rekodi mpya ya dunia

  (GMT+08:00) 2018-09-17 10:37:17

  Mwanariadha Eliud Kipchoge kutoka Kenya ameweka rekodi mpya ya Dunia katika mbio za marathoni baada ya kutumia muda mfupi zaidi kwenye ushindi wa mashindano ya Berlin aliopata jana.

  Kipchoge alitumia saa 2 dakika 1 na sekunde 39 na akivunja rekodi ya marathoni duniani iliyowekwa mwaka 2014 na mkenya mwingine Dennis Kimeto aliyetumia saa 2 Dakika 2 na sekunde 57.

  Licha ya kuvunja rekodi, Kipchoge pia alitetea ubingwa wake katika mbio hizo za Berlin kwani mwaka jana pia ndiye aliyeibuka mshindi.

  Katika mbio hizo za Berlin, mshindi wa pili na mshindi wa tatu wote ni kutoka Kenya, Amos Kipruto na Wilson Kipsang.

  Kwa upande wa wanawake Kenya imetamba pia, kwani mshindi wa kwanza katika mbio za Berlin ni Gladys Cherono aliyetumia muda wa saa 2, dakika 18 na sekunde 10, akiwatangulia Waethiopia wawili Ruti Aga na Tirunesh Dibaba ambaye ndiye alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako