• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Kimataifa wazungumzia maendeleo ya China

    (GMT+08:00) 2018-09-17 17:05:05

    Kongamano maalumu la baraza la ngazi ya juu la maendeleo ya China lilifanyika jana mjini Beijing, na wajumbe karibu 800 kutoka sekta ya viwanda, vyuo vikuu na serikali duniani wametoa maoni kuhusu maendeleo na mageuzi ya China katika zama mpya.

    Bw. Robert Bruce Zoellick aliyekuwa mkuu wa Benki ya Dunia amesema, China imepata maendeleo makubwa, na inafanya harakati kubwa zaidi duniani ya kupunguza umaskini. Katika miaka 40 iliyopita, China imewasaidia watu milioni 700 kuondoana na umaskini, na kuongeza maisha ya watu kuwa miaka 76.7 ya mwaka jana kutoka miaka 67.8 ya mwaka 1981. Mwaka jana wastani wa pato la kila mtu mmoja kitaifa ulifikia karibu dola 9,000 za kimarekani. Hata hivyo, China bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali. China inashika nafasi ya 70 kwa ukubwa wa wastani wa pato la kila mtu mmoja lakitaifa, na hadi mwishoni mwa mwaka jana, nchini China bado kuna watu maskini zaidi ya milioni tatu. Bw. Zoellick amesema changamoto hizo pia ni pamoja na namna ya kutimiza maendeleo endelevu na shirikishi. Ametaja kiwango cha mchango wa kampuni binafsi kwa maendeleo ya uchumi wa China. Kiwango hicho kilizidi asilimia 70, lakini kutokana na utatanishi wa hali ya kimataifa, hivi sasa kiwango hicho kimeshuka na kuwa asilimia 60. Hivyo serikali ya China inahitajiwa kufanya mageuzi mapya ili kuzisaidia kupata maendeleo zaidi.

    Miaka 40 iliyopita, uchumi wa China ulishika asilimia 1.8 tu ya uchumi wa dunia, na mwaka jana kiwango hicho kiliongezeka na kuwa asilimia 15. Ikiwa nchi ya kwanza kuuza bidhaa nje na nchi ya pili kuagiza bidhaa, China pia imezinufaisha nchi nyingine kutokana na maendeleo yake makubwa. Meneja mkuu wa Kampuni ya BMW ya Ujerumani Bw. Jochen Goller amesema, soko la China ni muhimu zaidi kwa kampuni za kutengeneza magari ikiwemo BMW. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana, idadi ya magari yaliyouzwa na BMW nchini China ilifikia laki 5.6, na ni kubwa zaidi kuliko idadi ya jumla ya mauzo nchini Marekani na Ujerumani ambazo zinashika nafasi ya pili na tatu baada ya China. Bw. Goller amesema, China pia imekuwa injini muhimu ya uvumbuzi duniani. mwaka huu, BMW itaanzisha vituo vipya viwili vya uvumbuzi nchini China.

    Bw. Lin Yifu aliyekuwa mwanauchumi mkuu wa Benki ya Dunia anaona kuwa, China inapaswa kubeba majukumu mengi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya dunia, na kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea katika juhudi za kujiendeleza na kupunguza umaskini ili kupata mafanikio ya pamoja. Bw. Lin ameongeza kuwa katika mchakato wa maendeleo, China itatoa ajira milioni 85 kwa nchi nyingine zinazoendelea, na kuzisaidia nchi hizo kuongeza uwezo wa utengenezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako