• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania imepata mikopo wa dola bilioni1.46 kutoka  Stanchart

    (GMT+08:00) 2018-09-17 19:37:25
    Tanzania imepata mkopo wa dola bilioni 1.46 kutoka kwa Shirika la Standard Chartered Bank ili kufadhili reli ya kati ya Morogoro na Dodoma.

    Waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango amesema mkopo mpya ulikuwa sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na mkurugenzi mtendaji wa Standard Chartered Bank Group huko Dar es Salaam, ambayo ingeweza kufadhili km 430 kati ya Morogoro na Makutupora.

    Tayari, serikali imetenga dola milioni 700 kwa miradi yake ya SGR katika bajeti ya mwaka 2018/2019.

    Tanzania inatarajia kutumia karibu na dola bilioni 14 kwenye reli hiyo kutoka mji mkuu hadi mpaka wake na Rwanda huko Rusumo, yenye kilomita karibu 2,600.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako