• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashirikiana na Namibia katika kujenga mgodi wa uranium na kunufaishana katika "Ukanda Mmoja Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2018-12-28 14:23:33

    Mwezi Mei mwaka 2012, Kampuni ya madini ya uranium ya Shirika la nishati ya nyuklia la China CGN ikishirikiana na Mfuko wa maendeleo ya China na Afrika CAD imefanikiwa kununua Mgodi wa uranium wa Husab wa Namibia, kitendo ambacho kimeufanya mradi huo uwe mradi mkubwa zaidi wa uwekezaji wa China barani Afrika. Mgodi huo ulianzishwa mwishoni mwa mwaka 2012, na kuzalisha pipa la kwanza la uranium tarehe 31 mwezi Disemba mwaka 2016, na katika mwaka 2017 kiwango cha uzalishaji wa uranium kimefikia tani 1,345. Mradi huo wa mgodi wa uranium wa Husab nchini Namibia umeweka muujiza wa kunufaishana katika Jangwa la Namib.

    Mradi wa mgodi wa uranium wa Husab umekuwa alama maarufu ya Namibia hivi leo, ambao unachangia sana katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi nchini humo. Meneja mkuu wa idara ya ushirikiano wa kimataifa katika Shirika la nishati ya nyuklia la China CGN Bw. Shi Weiqi anasema,

    "Ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Disemba mwaka 2012, ambapo umeweza kuipatia Namibia nafasi takriban 6,000 za ajira za muda kwenye kipindi cha ujenzi, na kuipatia nafasi 1,600 za ajira za kudumu kwenye kipindi cha uzalishaji. Kiasi cha uzalishaji wa ranosouranic oxide kinaweza kufikia tani takriban 6,500 kila mwaka, ambacho kitahimiza kiwango cha uuzaji wa bidhaa nje wa Namibia kiongezeke kwa asilimia 20, na pato la taifa liongezeke kwa asilimia 5 hivi. Mbali na hayo, Namibia inatarajia kuwa nchi ya pili duniani inayozalisha na kuuza nje bidhaa ya uranium, na nguvu ya ushindani ya Namibia kwenye sekta ya madini duniani pia itaongezeka. Mgodi wa uranium wa Husab unaendelea vizuri na kupata mafanikio katika jamii, umekuwa ishara ya kupendeza na jukwaa la kuonyesha matokeo ya maendeleo nchini Namibia."

    Naibu meneja mkuu wa upande wa Namibia katika Mgodi wa uranium wa Husab Bw Percy Mc Callum amesema mafanikio yanayopatikana hivi leo yanatokana na kushirikiana na kufundishana kati ya wafanyakazi wa Namibia na China.

    "Mgodi wa uranium wa Husab ni muhimu sana kwetu sisi. Nchi zetu mbili zinashirikiana vizuri kwenye ujenzi wa mradi huo, uhusiano wa ushirikiano kati ya wafanyakazi wa nchi mbili ni wa karibu siku zote. Kampuni yetu inashikilia wazo la 'kuheshimu utamaduni wa aina tofauti', tunafundishana, kushirikiana, kuelewana, kupata maendeleo kwa pamoja na kuifanya kampuni yetu iwe kundi lenye masikilizano. Kwa hivyo, tunaamini kuwa Mgodi wa uranium wa Husab utakuwa mradi mzuri zaidi duniani kote. Ingawa tunatoka suhemu tofauti duniani, lakini tunajizatiti kwa pamoja ili kutimiza lengo letu la uzalishaji."

    Katika ujenzi na uendeshaji wa Mgodi wa uranium wa Husab, kampuni hiyo ya China inashikilia wazo la kuwafundisha wafanyakazi wenyeji na kuwapatia mbinu za kazi. Mafundi wa China wanawafundisha wafanyakazi wa Namiba kwa makini ili kuwaandaa mafundi wenyeji. Kwa mfano, katika mchakato wa kupima kiasi cha uranium iliyomo ndani ya madini, kigezo cha upimaji huo kitaathiriwa na kiasi cha maji yaliyomo kwenye shimo lililotobolewa na mashine. Mhandisi wa China Bw. Chen Ning amewafundisha wafanyakazi wenyeji kwa kutumia akili zake zote, ili kuwafahamisha umuhimu wa mambo hayo.

    "Kwa mfano, mwanzoni kulikuwa na maji ndani ya shimo, hivyo walilazimika kupima kina cha maji. Lakini wafanyakazi wengi hawakufanya hivyo. Nikawaambia mstari wa Gamma utakapotokea kwenye madini, utafyonzwa na maji, hivyo idadi hiyo lazima irekebishwe tutakapohesabu. Kisha wakanifahamu na kuanza kupima kina cha maji kama nilivyofanya."

    Licha ya hayo, wafanyakazi wa Namibia wamepata mambo mengi zaidi kwenye kazi zao. Meneja wa Mgodi wa uranium wa Husab anayeshughulikia mambo ya mafunzo na maendeleo Bi. Sophy Partenbach Fick anaona kuwa utamaduni wa kipekee wa Shirika la nishati ya nyuklia la China CGN unaweza kuwahimiza wafanyakzi waendelee siku hadi siku. Kipindi chake cha kufanya kazi hapa kitakuwa kumbukumbu isiyosahauliwa.

    "Miaka mitano imeshapita tangu nilipoanza kufanya kazi kwenye kampuni hii mwaka 2013. Muda huo wa miaka mitano umekuwa safari ya kupendeza maishani mwangu. Nikiwa ni mfanyakazi mmojawapo wa kampuni hiyo, nashuhudia changamoto zinazoukabili mradi huo. Wafanyakzi wa kampuni hiyo wanatoka sehemu mbalimbali zenye utamaduni wa aina tofauti, ambao wanaipatia kampuni yetu mazingira ya kipekee. Kwa hivyo, tunapaswa kuelewana na kuwa kundi moja lenye ufanisi. Utamaduni na msimamo wa thamani katika kampuni yetu unatuhimiza kusonga mbele. Naamini kwamba mgodi wetu wa uranium utashinda ugumu na changamoto yoyote. Kwa hiyo, naona nimepata uzoefu wa kupendeza wenye uchangamfu kutokana na kazi yangu."

    Uhusiano wenye masikilizano katika jamii ni sababu nyingine muhimu inayosaidia Shirika la nishati ya nyuklia la China litekeleze mradi wake nje ya nchi bila vizuizi. Kampuni yake ya madini ya uranium imefanya shughuli nyingi za kiutamaduni na za kusaidia jamii nchini Namibia. Naibu meneja wa idara ya mpango na uhandisi katika Mgodi wa uranium wa Husab Bw. Gao Junli anasema,

    "Tumebeba majukumu mengi ya kijamii kwa hiari. Kuna mambo mawili muhimu: La kwanza, tulishirikiana na serikali ya mtaa katika kufanya hafla ya Siku ya kuhifadhi mazingira mjini Swakopmund, ambayo tuliwasaidia wakazi wa huko kuwakusanya katikati na kuwaletea vifaa vya usafishaji, walitukaribisha sana. La pili, tunafanya michezo ya Marathon huko Husab kila mwaka, imekuwa michezo mikubwa zaidi nchini Namibia, ambayo ni fursa nzuri ya kuonyesha sura ya Husab kwa Namibia na hata kwa dunia nzima. Mbali na hayo, tunazingatia sana uhifadhi wa mazingira. Kwa mfano, kuna aina ya mmea maalum uitwao welwitschia mirabilis kwenye Jangwa la Namib. Wakati tulipojenga kiwanda chetu tulichukua hatua nyingi za kuhifadhi mmea huo. Hadi sasa, idara yetu ya kuhifadhi mazingira bado inafanya uchunguzi kwa mfululizo kwenye maeneo yenye mmea huo, na imesifiwa na serikali ya huko."

    Mwenyekiti wa Shirika la nishati ya nyuklia la China CGN Bw. He Yu ameeleza kwamba Mgodi wa uranium wa Husab unatarajiwa kutimiza lengo la uzalishaji kamili ndani ya mwaka 2018. Mradi huo utaipatia Namibia nguvu mpya katika maendeleo ya uchumi usiosababisha uchafuzi, pia utainufaisha jamii na wakazi wa huko, na kuhakikisha utoaji wa mafuta kwa ajili ya mashine ya uzalishaji wa umeme wa nyuklia, kitendo ambacho kinasaidia kujenga imani katika maendeleo ya shughuli za umeme wa nyuklia ya China yenye usalama na ufanisi, pia kinaweza kuonyesha sifa ya kushirikiana na kunufaishana kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja Njia Moja".

    Juu ya matokeo yanayopatikana na mpango wa siku za usoni, Meneja mkuu wa idara ya ushirikiano wa kimataifa katika Shirika la nishati ya nyuklia la China CGN Bw. Shi Weiqi anasema,

    "Maendeleo ya Shirika la CGN yanaambatana na maendeleo ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China. Mwanzoni shirika letu lilijitahidi kujifunza mambo ya nje na kupata maendeleo hatua kwa hatua, hadi sasa tunaweza kumaliza vizuri kazi tunazopewa na taifa letu. Kwa mujibu wa pendekezo la 'Ukanda Mmoja Njia Moja', tutaijulisha dunia teknolojia, uzoefu, vifaa, huduma na utawala kwenye umeme wa nyuklia wa China, ili kutoa mchango wetu katika maendeleo ya sekta ya umeme wa nyuklia ya dunia."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako