• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China apongeza kuanza kwa mkutano wa kimataifa wa akili bandia wa mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-09-17 20:53:31

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya kupongeza kuanza kwa Mkutano wa kimataifa wa akili bandia wa mwaka 2018 huko Shanghai.

    Katika barua hiyo, Rais Xi amewakaribisha watu wa sekta mbalimbali wanaohudhuria mkutano huo wakiwemo wajumbe wa nchi mbalimbali, wakuu wa mashirika ya kimataifa, wataalam, wasomi na wafanyabiashara. Amesema teknolojia mpya ya akili bandia inaleta ustawi wa dunia, kuongeza nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi na jamii, na inabadilisha njia ya uzalishaji na maisha ya watu. Nchi mbalimbali zinapaswa kuzidisha ushirikiano na kufanya majadiliano kwa pamoja kwa ajili ya kutumia fursa hiyo na kutatua masuala mapya ya matumizi ya akili bandia katika sekta ya sheria, usalama, ajira, maadili na usimamizi ya serikali. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kusukuma mbele maendeleo, kulinda usalama na kugawanya mafanikio katika sekta ya akili bandia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako