• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tennis ya meza: Mikakati ya kuuboresha yaanza huko Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-09-18 09:24:18

    Chama cha mchezo wa tennis ya meza cha Zanzibar kwa kushirikiana chama cha mchezo huo cha Tanzania Bara kwa pamoja vimejipanga kuhakikisha mchezo huo unakuwa na wachezaji wengi wa kushindana katika mashindano ya kimataifa.

    Moja ya mipango hiyo ni semina iliyoandaliwa kwa pamoja kwa kushirikiana na kamati ya Olimpiki ya Tanzania kwa lengo la kutoa mafunzo ya mchezo huo.

    Mafunzo hayo yalitolewa kwa wakufunzi saba kutoka Zanzibar na Tanzania bara ili kuwapa ujuzi wa kuelewa mchezo huo kwa kuwa ndio mabalozi wazuri kwa wanafunzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako