• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rugby: Kenya kucheza dhidi ya Romania na Namibia kabla ya mchujo wa kombe la Dunia

    (GMT+08:00) 2018-09-18 09:25:45

    Timu ya taifa ya mchezo wa Raga ya Kenya itacheza mechi nne za kujipima nguvu Oktoba 7 na Novemba 3 kabla ya mchujo wa kufa na kupona wa kufuzu kushiriki kombe la dunia la raga ya wachezaji 15 itakayofanyika nchini Ufaransa kuanzia Novemba 11 hadi 23 mwaka huu.

    Shirikisho la mchezo wa raga nchini Kenya (KRU) limesema timu hiyo itamenyana na timu za Namibia na Romania kabla ya kuelekea mjini Marseille.

    Simbas itamenyana na Canada, Hong Kong na Ujerumani katika mchujo wa kuingia Kombe la Dunia. Mshindi wa mchujo huo wa mataifa manne atajaza nafasi ya 24 ambayo ni nafasi ya mwisho iliyosalia na kupangwa kundi kundi B pamoja na New Zealand, Afrika Kusini, Italia na Namibia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako