• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa Baraza la Uchumi la Dunia ana imani juu ya ongezeko la uchumi la China

    (GMT+08:00) 2018-09-18 10:07:44

    Mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa Baraza la Uchumi la Dunia Bw. Klaus Schwab amesema, siku zote ana imani juu ya ongezeko la uchumi la China.

    Bw. Schwab anaona wakati mapinduzi ya nne ya kiviwanda yakiendelea, uvumbuzi umechukua sehemu muhimu katika nguvu za ushindani. Hivi sasa China iko katika njia ya maendeleo katika kujenga jamii yenye uvumbuzi, na inatakiwa kuandaa waanzishaji wengi wa biashara, kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu, na kuwanufaisha zaidi wananchi.

    Bw. Schwab pia anakaribisha pendekezo la China kuhusu "Ukanda mmoja, Njia moja", akisema kutokana na pendekezo hilo miundombinu duniani itaungana, na nguzo kwa kufanya mapinduzi ya nne ya kiviwanda ni ushirikiano wa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako