• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuzidisha vita ya biashara na China hakutasaidia utatuzi wa suala

    (GMT+08:00) 2018-09-18 17:49:51

    Marekani imetangaza kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 10 kwa bidhaa kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 200 za kimarekani kuanzia tarehe 24, na kutishia kuchukua hatua zaidi dhidi ya China. Wizara ya biashara ya China imeeleza masikitiko makubwa, na kusema China itajibu hatua hiyo ya Marekani kwa wakati mmoja.

    Wachambuzi wanaona kuwa bila kujali Marekani inafanya nini, China ina nia na uwezo wa kutosha katika kulinda maslahi ya taifa na wananchi, na utaratibu huria wa biashara wa pande nyingi.

    Kwanza, katika orodha ya bidhaa inazoagiza Marekani kutoka China, nyingi hazihusiani na maslahi ya China, huku zikiwa na athari kubwa kwa wateja wa Marekani. Kipindi cha manunuzi cha Krisimasi kinakaribia kufika, ongezeko la ushuru wa forodha kwa bidhaa za China litaleta athari kubwa kwa wateja wa Marekani. Hivyo mashirikisho mengi ya wafanyabiashara ya Marekani yameeleza kupinga serikali yao kufanya hivyo. Mkuu wa taasisi ya utafiti wa uchumi wa kimataifa ya Peterson Bw. Adam Posen amesema, uamuzi wa serikali ya Donald Trump wa kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za nje utashindwa.

    Pili, China ilitangaza hatua ya kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola bilioni 60 za Kimarekani mwanzoni mwa mwezi Agosti ili kujibu hatua ya Marekani, na kuonesha kuwa itachukua hatua zaidi zinazolingana na uamuzi wa Marekani katika suala la biashara.

    Tatu, kiwango cha umuhimu wa biashara ya kimataifa katika uchumi wa China kimeshuka na kuwa asilimia 33.7, na kuonesha kuwa ongezeko la uchumi wa China litategemea zaidi matumizi na uwekezaji wa ndani. Aidha, China ina watu bilioni 1.4, sekta kamili za viwanda, mifumo bora na mkakati thabiti wa ufunguaji mlango, na inaweza kukabiliana na changamoto yoyote ya nje, na kuendelea kushughulikia vizuri mambo yake.

    Rais Donald Trump amesema akiwa rais wa Marekani, kulinda maslahi ya wananchi ni jukumu lake, lakini alipotoa uamuzi wa kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa kutoka China, amepuuza malalamiko ya kampuni zake. Biashara inanufaisha pande zote za China na Marekani, na ushirikiano ni njia pekee iliyo sahihi kwa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako