• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka pande mbalimbali zishirikiane kuhimiza mchakato wa amani wa peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2018-09-18 19:07:33

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amezitaka pande mbalimbali zishirikiane kuimarisha hali ya utulivu ya mazungumzo kuhusu peninsula ya Korea, kuhimiza mchakato wa amani na kutimiza usalama wa kudumu kwenye peninsula hiyo.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea hapo jana, Balozi Ma amesema, China inaunga mkono mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini ili kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea. Amesema China inaziunga mkono Korea Kaskazini na Korea Kusini kufanya mazungumzo na kuhimiza ushirikiano na maafikiano, ikiwataka viongozi wa nchi hizo mbili wapate mafanikio katika mazungumzo yanayofanyika huko Pyongyang. China inaisifu Korea Kaskazini kufanya juhudi kwa kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea na kulinda amani ya peninsula hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako