• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yailaumu Israel kwa kosa la Syria la kutungua ndege ya Russia

    (GMT+08:00) 2018-09-18 19:09:58

    Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema ndege ya nchi hiyo iliyobeba askari 15 ndani imetunguliwa kimakosa na kombora lililorushwa na Syria, lakini Russia inailaumu Israel kuwa chanzo cha kosa hilo.

    Msemaji wa Wizara hiyo Igor Konashenkov amesema, askari 15 wa jeshi la Russia wameuawa kutokana na vitendo visivyo vya kuwajibika vilivyofanywa na jeshi la Israel, na kwamba kitendo hiko hakiendani na moyo wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Ndege hiyo iliyokuwa njiani kurejea kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Hmeymim nchini Russia ilipotea kwenye rada jana usiku wakati ambao ndege nne za kijeshi za Israel ziliposhambulia maeneo yaliyolengwa mkoani Latakia, nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako