Katibu wa kudumu katika Ofisi ya Rais Stuart Comberbach alisema rasimu ya Mpango wa miaka miwili wa kiuchumi umetolewa kwa wadau ili kuzingatia.
Alisema mpango huo utaongoza uchumi kwa miaka miwili ijayo na utafuatiwa na mipango miwili ya maendeleo ya taifa ya miaka mitano.
Ameeleza kwamba ya kwanza itakuwa 2021 hadi 2025 na mwingine mwaka wa 2026 hadi 2030.
Utawala mpya wa Zimbabwe chini ya Rais Emmerson Mnangagwa unalenga kuwa uchumi wa katikati kipato cha dola bilioni 65 mwaka wa 2030.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |