• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima wa mpunga wataka soko zaidi nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2018-09-18 19:13:37
    Wakulima wa mpunga nchini Tanzania wameiomba Serikali kuondoa zuio la usafirishaji wa mchele nje ya nchi kutokana na kiasi kilichopo sasa cha ziada ya tani 1.2 milioni kukosa soko la uhakika la ndani.

    Wakulima hao walisema kukosekana kwa soko la uhakika kumefanya bei ya mchele kudorora na kuwasababishia hasara kwa sababu wanatumia gharama kubwa katika uzalishaji wake.

    Septemba 12, Serikali ilitoa agizo la kusitisha uagizwaji wa mchele kutoka nje ya nchi kutokana na uliopo nchini kutosheleza mahitaji.

    Ilisema mchele uliopo nchini kwa sasa ni tani milioni 2.2, kiwango kilichotokana na wakulima wa mpunga kupatiwa mbinu bora za kitaalamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako