• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya Airways kuzindiua safari mbili zaidi za kwenda Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-09-18 19:16:58

    Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways litazindiua safari mbili zaidi za kwenda Afrika Kusini kuanzia Novemba 20.

    Mwenyekiti wa shirika hilo Michael Joseph amesema hatua hiyo imechangiwa na kuongezeka kwa wasafiri wanaokwenda kutalii Afrika Kusini.

    Kuongezeka kwa safari hizo mbili kutafikisha tano idadi ya safari za shirika hilo kwa kutumia ndege aina ya Boeing 737-800.

    Mtandao wa utalii wa Afrika Kusini, Wesgro, umekaribisha hatua hiyo na kusema Kenya iko kwenye nafasi ya nne kwa soko la watalii wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako