• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua hatua ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani kuanzia terehe 24 Septemba

    (GMT+08:00) 2018-09-18 21:39:45

    Wizara ya Fedha ya China imesema, kitendo cha Marekani kimesababisha kuongezeka kwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani.

    Ili kulinda biashara huria na utaratibu wa pande nyingi, na kulinda maslahi yake halali, China inalazimika kuchukua hatua ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 60.

    Kwa mujibu wa sheria ya biashara ya kimataifa ya China, kanuni ya ushuru ya uuzaji wa bidhaa kwa nje na uagizaji bidhaa kutoka nje, na sheria nyingine za China, Baraza la Serikali la China limeidhinisha kamati ya ushuru ya baraza hilo kuongeza ushuru kwa asilimia 10 na asilimia 5 dhidi ya bidhaa za aina 5,207 zenye thamani karibu dola za kimarekani bilioni 60, hatua hiyo itatekelezwa rasmi kuanzia tarehe 24 Septemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako