• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yailaumu Israel kusababisha ndege ya kivita ya nchi hiyo kuangushwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria

    (GMT+08:00) 2018-09-19 09:53:11

    Wizara ya ulinzi wa taifa ya Russia imesema, wakati ndege za kivita za Israel zikishambulia shabaha ya Syria, zilitumia ndege ya kivita ya Russia kuficha ya kwao. Hatua hiyo isiyowajibika imesababisha ndege ya kivita ya Russia kuangushwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria na wanajeshi 15 wa Russia kuuawa. Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imetoa taarifa ikisema, waziri mkuu Bw. Benjamin Netanyahu ametoa salamu za pole kwa wanajeshi waliofariki na kusema Syria inapaswa kuwajibika kwa kuangushwa kwa ndege ya kivita ya Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako