• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Ethiopia aahidi kuwakamata wahalifu waliohusika na tukio la kimabavu la kikabila lililotokea mwisho wa wiki iliyopita

    (GMT+08:00) 2018-09-19 10:09:59

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed ameahidi kuwakamata wahalifu waliohusika na tukio la kimabavu la kikabila lililotokea mwisho wa wiki iliyopita huko Burayu, kitongji cha Addis Ababa.

    Bw. Ahmed alisema hayo wakati alipokwenda kuwatembelea watu 900 hivi waliopoteza makazi yao kutokana na vurugu za Burayu. Zaidi ya watu 23 waliuawa kwenye shambulizi lililofanywa na watu wa kabila la Oromos dhidi ya watu wa makabila mengine wanaoishi Burayu.

    Bw. Ahmed pia aliahidi kuwa tukio kama hilo halitatokea tena, na serikali itafanya juhudi ili kuwasaidia watu waliopoteza makazi yao kurudi kwenye nyumba zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako